Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akitoka katika chumba cha mikutano baada ya
kuhudhuria kikao cha 29 cha wakuu wa nchi za NEPAD pembeni ya mkutano wa
maadhimisho ya miaka 50 ya AU katika makao makuu ya Umoja huo jijini
Addid Ababa, Ethiopia.
Wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika na wageni mashuhuri walioalikwa wakiwa
katika picha ya pamoja wakati wa mkutano wa maadhimisho ya miaka 50 ya
AU katika makao makuu ya Umoja huo jijini Addid Ababa, Ethiopia.
Marais wastaafu waliohudhuria maadhimisho ya miaka 50 ya AU katika
makao makuu ya Umoja huo jijini Addid Ababa, Ethiopia. Kutoka kushoto ni
Dkt Kenneth Kaunda (Zambia), Sam Nujoma (Namibia) na Mzee Festus Mogae
(Botswana).
Mama Salma Kikwete na wake wa marais wengine wakiwa katika mkutano wa
maadhimisho ya miaka 50 ya AU katika makao makuu ya Umoja huo jijini
Addid Ababa, Ethiopia.
Wapiga picha toka nchi mbalimbali wakiwa kazini wakati wa mkutano wa
maadhimisho ya miaka 50 ya AU katika makao makuu ya Umoja huo jijini
Addid Ababa, Ethiopia. (PICHA NA IKULU)
Post a Comment